JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA

BARAZA LA MASOKO YA MITAJI

MWENYEKITI WA BARAZA

Mhe. Jaji Dkt. Deo John Nangela

MSAJILI WA BARAZA

Mhe. Martin Wilbert Kolikoli

Huduma Zetu

Usuluhisho wa migogoro

Baraza likiwa kama taasisi inayojitegemea kwa ajili kusikiliza rufaa zinazotokana na migogoro kati ya washiriki wa masoko, wawekezaji, na Mamlaka katika masuala yote ya masoko ya mitaji na dhamana

⁠Utekelezaji wa kanuni

Baraza ikiwa ni taasisi inayojitegemea, lina jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria za masoko kwa kutoa adhabu kwa wadau ambao wamevunja taratibu za masoko kupitia maamuzi ya Baraza. Baraza lina mamlaka kamili ya Mahakama Kuu katika utekelezaji wa majukumu yake

⁠Mapitio ya maamuzi mamlaka

Baraza lina Mamlaka ya kupitia maamuzi yaliyotolewa na Mamlaka kuhusiana na masoko ya mitaji kwa lengo la kuhakikisha maamuzi hayo yanazingatia sheria na hayapo kinyume na haki za washikiri wa masoko

⁠Kutoa mwongozo

Baraza linatoa mwongozo na tafsiri ya sheria na kanuni za masoko ya mitaji kwa lengo la kuhamasisha uwazi na utii kati ya washiriki wa masoko